AKON APINGANA NA TAARIFA YA NELLY YA UBAKAJI

  Share this

  Baada ya kukumbwa na janga la kutuhumiwa kufanya Ubakaji siku ya jumamosi katika Tour bus ambayo huitumia katika ziara zake huko washington, Nelly aliamua kufunguka kwa mara ya kwanza kwenye kurasa yake ya Twitter kwa kusema kwamba hilo kosa amesingiziwa na nia nikulichafua jina lake.

  Kupitia mfululizo wa Tweets zake ambazo anawashukuru mashabiki wake kwa kuwa nae Bega kwa bega na kumuamini kwamba hajafanya tukio hilo, Sasa Moja ya washikaji wake wa karibu, Akon ameamua kuongezea kwamba anamfahamu Nelly Muda mrefu na hadhani kama Nelly anaweza kufanya jambo kama hilo.

  Kupitia video ambayo imepostiwa na mtandao wa Tmz inamwonyesha Akon akifunguka na kutoa maoni yake kuhusu Ishu hiyo ambayo imemgusa kila mtu na kumake headline kwa tukio hilo la Nelly.

  Dondosha comments


  Share this