ALICHOKISEMA DAKTARI WA LIL WAYNE BAADA YA MSANII HUYO KUANGUKA NA KIFAFA

  Share this

  Taarifa mbaya kutoka katika tasnia ya muziki ni kwamba msanii na member wa kundi la Young Money Lil Wayne amepata tatizo la kuanguka ghafla akiwa hotelini ambako alifikia kabla ya kwenda kufanya show yake huko Las Vegas.

   

  Wayne ambaye siku ya jana alikuwa na tamasha lake katika ukumbi wa Drais Beach club mjini Vegas,Tamasha hilo limekatishwa  baada ya msanii huyo kukutwa akiwa hana fahamu na ikaelezwa kuwa ameanguka kutokana na ugonjwa wa kifafa.

  Image result for LIL WAYNE

  Kwa mujibu wa vyanzo viwili vya karibu zimeeleza kuwa rapper huyo amelazwa  katika hospitali ya Northwestern Memorial iliyopo mjini Chicago baada ya kukutwa amepoteza fahamu katika chumba cha hotel cha Westin Michigan Avenue.

  Kwa mujibu wa Daktari aliyekuwa akimtibua msanii huyo amemtaka apumzike kwa siku kadhaa ili afya yake iweze kurudi katika hali ya kawaida licha ya kuwa aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo siku ya jana hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyo kuugua na kuanguka kutokana na ugonjwa wa huo, pia msanii huyo aliwahi kukiri kuwa anatumia dawa za kuzuia hali hiyo isitoke mara kwa mara.

  Image result for LIL WAYNE

  Dondosha comments


  Share this