Alichokisema Q Chief baada ya WCB kutambulisha msanii mpya

  Share this

  Ukithrowback miezi kadhaa nyuma utakutana na story zinazomuhusisha mkali na mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Abubakar Katwila almaaruf Q Chief kuhusu kufanya kazi na lebo ya WCB Wasafi.

  Story ambazo zilikwenda mbali zaidi na kusemekana kuwa huenda Q Chief akadondosha wino katika lebo hiyo ya WCB.

  Jana kwenye Leo Tena ya Clouds fm WCB Wasafi walimtambulisha msanii wao mpya ambaye anafahamika kwa jina la Lava Lava, na maswali mengi yalikuja vichwani mwa watu ikiwa wengine walitegemea huenda angekuwa Q Chief.

  Perfect255 imepiga storyna Q Chief na ameelezea mtazamo wake juu ya WCB kumtambulisha msanii huyo mpya.

  “WCB is an organization, is an institute of many people with many creativity and have done alot of things, and i respect that, lakini wao wako chini kukaa na kufikiria nini wafanye kuhusu mimi, na mimi nina mambo yangu, siwezi kuacha kwasababu wao wanafikiria, all i know ni kwamba this music is growing, watu wasubiri project yangu mpya.” Alisema Q Chief.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini ili uweze kumsikiliza Q Chief akiongelea mustakabali wa yeye kujiunga na WCB.


  • Full interview ya WCB Wasafi wakimtambulisha msanii wao mpya kwenye Leo Tena ya Clouds fm.

  Dondosha comments


  Share this