Alichokisema Rayvanny baada ya kutajwa kuwania International Viewr’s Choice Awards

  Share this

  Jana May 15 zimetangazwa category za wanaowania tuzo za kituo cha televisheni cha Black Entertainment cha nchini Marekani (BET).

  Ni Mtanzania mmoja tu ambaye ametajwa kwenye tuzo hizo, Rayvanny wa WCB Wasafi. Akiwa kama mwakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki, Rayvanny ametumia ukurasa wake wa instagram kuonyesha furaha yake na kutoa shukrani kwa wote ambao anaamini wana mchango katika kulifanikisha hili

  Kupitia ukurasa wake wa instagram, Rayvanny ameandika Mungu Anamipango Yake Na Usipokata tamaa Kwenye Maisha Mafanikio Utayaona Ni Mwaka Tu Umepita nilipotambulika Kwenye Ramani Ya Mziki.Lakini kwa Baraka Za mwenyez Mungu Kazi Kubwa Ya Uongozi wangu #WCB Na Wadau Na Mashabiki Wote Mnaonisapoti.Huu Ni Mwanzo tu Bado Naitaji Sana Sapoti Yenu Ndugu Zangu #betawards2017 God is good all the time #InternationalViewersChoiceAward

  Pia Perfect255 imemvutia waya Rayvanny na kupiga naye story kuhusiana na suala hilo la yeye kuchaguliwa kuwania tuzo hiyo. Kusikiliza alichokisema Rayvanny bonyeza play kwenye video hii hapa chini.


   

  Dondosha comments


  Share this