Alikiba kufumua DUDE jipya alilofanya na Producer Man Water

  Share this

  Unaikumbuka ile Mwana? Ngoma ambayo ilimrudisha vyema kabisa kwenye game ya music mfalme wa Bongo fleva Ally Saleh Kiba baada ya kimya cha muda mrefu.

  Kama hukumbuki vyema, ninachotaka kukukumbusha saa hii ni kwamba ngoma ile (Mwana) ilisukwa na mtayarishaji mkali na mkongwe wa Bongo fleva, Man Water.

  Kama ulimiss aina na ladha ya muziki kama ule kutoka kwa King Kiba, the wait is over, sababu ametusanua kuwa yuko katika hatua za mwisho kuikamilisha ngoma yake mpya ambayo amefanya tena na producer Man Water hitmaker wa Mwana.

  Kupitia Snapchat, Alikiba amesikika akisema kuwa “Yani hapa niko studio katika ku-finalize BALAA, niko na Producer Man Water.”

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini kumtazama na kumsikiliza Alikiba akifunguka juu ya balaa lake hilo jipya na producer Man Water.

  Kwa ukubwa wa ngoma ya Mwana, uwezo wa Alikiba kwenye muziki na ukali wa Man Water ni haina ubishi kuwa ngoma hiyo tayari ni hit.

  Dondosha comments


  Share this