Baada ya Wema Sepetu, Wolper kuja na App yake!

  Share this

  Kufuatana na teknolojia inavyozidi kukua siku hadi siku na dunia nzima kuonekana kuelekea huko, mastaa wetu kibongo bongo wameonekana kutobaki nyuma kwa kutumia fursa ambazo wanazipata kutokana na majina yao na vitu kama hivyo.

  Baada ya TZ Sweetheart Wema Sepetu kufungua application yake ya simu za mikononi (Smartphones) na kuwa wezesha mashabiki zake kupata habari zake kwa haraka zaidi na kujiweka karibu nao muda wote kwa kuchat na mengineyo, Jacqueline Wolper kutoka katika kiwanda cha Bongo Movie pia ametusanua tukae mkao wa kula kuipokea application yake pia.

  Kupitia ukurasa wa instagram wa Jacqueline Wolper niliyanyaka baadhi ya maneno kwenye moja kati ya captions ndefu ambazo anapost mrembo huyo kwenye page yake hiyo.

  Maneno “Nina mengi sana nitayaongea NIKIZINDUA APP YANGU verry soon mtajua kila kitu kuliko uwongo unaoendelea kusambaa bila huruma” kwenye caption ya moja kati ya posts za Wolper July 29 yalitosha kuniaminisha kuwa mrembo huyo amedhamiria kuwaletea mashabiki zake App itakayo muweka nao karibu.

  Dondosha comments


  Share this