Bado nashoot video nje kwasababu natafuta Ubora-: Joh Makini

  Share this

  Pampja na kuwa sekta ya production inazidi kukua siku hadi siku hapa Bongo, kutokana na madirector wa hapa kujiongeza na kufanya vitu vikali siku hadi siku na hata kupelekea video za hapa kuchezwa kwenye vituo vyote vikubwa Afrika, bado imani ya Joh Makini haijawa rafiki kwa madirector wa hapa nchini kiasi cha kuwaamini na kufanya nao kazi.

  Mkali huyo wa muziki kutoka kaskazini amedai kuwa kitu pekee ambacho kinamfanya asafiri na kwenda kufanya kazi na madirector wa nje ni ubora, Joh amedai ubora ambao anaupata akiwa nje, hana imani kama ataupata kwa madirector wa ndani japo kuwa wanazidi kukua siku hadi siku.

  “Siwezi kuficha kwamba natafuta ubora, na standard ambayo nimeset katika muziki wa Joh Makini inanilazimisha kuendelea kwenda juu na sio kurudi chini, nawaamini madirector wa ndani ila kusema ukweli nakuwa comfortable nikifanya kazi na madirector wa nje kwasababu nakuwa sina stress nakuwa napata kitu ambacho nimeset na wao wanakuwa wanafanya kitu ambacho very professional” Alisema Joh Makini.

  Pia Joh Makini aliongeza kuwa “Sina maana kuwa wa nyumbani sio professional, ila nafkiri wenyewe wanaelewa kuwa wanatakiwa wajipange zaidi ili waweze kwenda sambamba na ukubwa wa wasanii wao wa nyumbani ambao wako kwenye international level, lakini so far wanafanya kazi nzuri.”

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini uweze kumsikiliza Joh Makini akifunguka kuhusiana na issue hiyo mwanzo mpaka mwisho.

  Ukimsikiliza vizuri Joh Makini kwenye video hiyo utasikia akisema kwamba soon wataacha kusafiri kwasababu ya madirector, na labda pengine kufuata locations na vitu kama hivyo.


   

  Dondosha comments


  Share this