Barnaba ajitolea kumsaidia Hawa wa Nitarejea

  Share this

  Ijumaa iliyopita kwenye kipindi cha D’Weekend Chat Show cha Clouds TV maarufu kama Shilawadu kilirusha taarifa za binti afahamikaye kama Hawa aliyewahi kushirikishwa na msanii Diamond Platnumz kwenye wimbo wa Nitarejea miaka kadhaa iliyopita.

  Binti ambaye alionekana kugusa nyoyo za wengi kutokana na kuathirika kwake na matumizi ya pombe za kienyeji na kuomba msaada kwa ambao wana uwezo wa kumsaidia kuondokana na hali hiyo waonyeshe huruma zao.

  Mmoja kati ya Wasanii ambao waliguswa kinamna yake na story ya mwanadada huyo ni pamoja na hitmaker wa Lover Boy Barnaba Classic ambaye amepiga story na Social Buzz ya Clouds TV na kudai kuwa jambo la kwanza ambalo atahakikisha ni kumsaidia Hawa kuondokana na matumizi ya pombe za kienyeji.

  “Mimi Hawa ni dada yangu, na kutokana na ambacho nimekisikia ni lazima na mimi mwenyewe nifanya mpango wa kuonana na dada yangu ila all and all mimi ni mtu wa msaada na ninasapoti popote ambapo naweza ila chakwanza nitahakikisha kwanza afya yake inakaa sawa.” Alisema Barnaba

  Dondosha comments


  Share this