BET Awards 2017, yafufua bifu la Remy Ma na Nicki Minaj

  Share this

  Tumeshuhudia disstrack kibao kutoka pande zote mbili na majigambo tofauti, BET Awards 2017 imekuja kufufua bifu la Nicki Minaj na Remy Ma upya kwa mashabiki.

  Image result for Nicki Minaj vs Remy Ma

  Wakati wa Bifu la Minaj na Remy Ma, kila shabiki alitega sikio lake kusikiliza nani anamuumiza mwenzake kwa punch kali za disstrack zenye maneno yaliyoshiba, wengine walikuwa upande wa Remy Ma na wengine kwa Minaj,licha ya Remy Ma kuwahi kufunguka kwamba bifu lao kashalitupilia huko, mashabiki bado wanahamu nani atavaa urap queen katika game ya Hiphop kwenye tuzo hizi za BET

  Kama utakumbuka, Nicki Minaj ameshachukua tuzo ya hiyo tangu 2010, wapo wengine ambao wanaangaliwa katika kipengele hicho kama, Missy Eliot, Young M.A pamoja na cardi B, ila hamu imejaa kwa Remy Ma na Nicki katika tuzo hizo za BET 2017.

   

  Dondosha comments


  Share this