BREAKING NEWS: Baraka Da Prince afunguka rasmi kujitoa Rockstar 4000

  Share this

  Kitaani kulikuwa na tetesi kuhusu kutokuwepo kwa maelewano mazuri baina ya wasanii wawili wa Bongo fleva ambao walionekana kuwa na ukaribu mkubwa siku za nyuma.

  Ni Baraka Da Prince na Alikiba ambao wote walikuwa chini ya uongozi wa record label ya Rockstar 4000, ikiwa ni kabla ya siku chache zilizopita Alikiba kutangazwa kama mmoja kati ya body ya ma-director wa lebo hiyo.

  Baraka Da Prince alifanya interview na kipindi cha Ala za Roho cha Clouds fm na kufunguka kuwa hatambui nafasi ambayo amepewa msanii Alikiba katika uongozi wa lebo ya Rockstar  kutokana na kuwa hajafahamishwa na vitu kama hivyo na kudai kuwa ni vitu ambavyo anaviona kwenye mitandao ya kijamii tu.

  Gumzo ndio likaanzia hapo na utofauti wa Baraka Da Prince na Alikiba ukawa hadharani baada tu ya usiku huo kumaliza interview na Ala za Roho.

  Leo kwenye XXL ya Clouds fm Baraka Da Prince ame break the news kwamba hayuko tena chini ya uongozi wa lebo ya Rockstar 4000 kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na uongozi wa lebo hiyo.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini uweze kumsikiliza Baraka Da Prince mwenyewe kwa mdomo wake akifunguka juu ya suala hilo.

  Dondosha comments


  Share this