BREAKINGNEWS: Dogo Mfaume wa “Kazi ya Dukani” amefariki Dunia

  Share this

  Leo kwenye 255  ya XXL kulikuwa na taarifa ambayo sio nzuri kumuhusu aliyekuwa mkali wa muziki wa Mnanda Dogo Mfaume aliyejizolea umaarufu mkubwa na wimbo wake wa kazi ya dukani.

  Taarifa ambayo ilikuwa ikidai kwamba Dogo Mfaume anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwenye kichwa kutokana na kuwa na uvimbe karibu na ubongo.

  Muda sio mrefu zimeripotiwa taarifa kuwa hatunaye tena duniani Dogo Mfaume, imeripotiwa kuwa Dogo Mfaume amepoteza maisha katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa kwa matibabu kama kuongezewa damu na Ijumaa kufanyiwa Upasuaji.

  Mungu ailaze roho ya marehemu Dogo Mfaume mahali pema peponi amina.


   

  Dondosha comments


  Share this