Bushoke ajipanga kujikita kwenye Biashara hii mwaka huu 2017

  Share this

  Kila mmoja amejipangia mipango na malengo yake kwa mwaka huu mpya wa 2017 akiwa na nia ya kuyakamilisha na kuweza kusonga mbele kimaendeleo kama ilivyo matarajio ya kila mmoja.

  Kutoka Bongo Flevani mkongwe Bushoke ametusanua ni mipango gani ambayo yeye binafsi amejipangia kwa mwaka huu wa 2017.

  Bushoke ameiambia Perfect255 kuwa kwa mwaka huu wa 2017 amejipanga kujikita zaidi kwenye biashara ya kilimo na ufugaji ikiwa ni mipango yake ya siku nyingi lakini time hii ameamua kuichukulia serious.

  “2017 nataka niwe mkulima na mfugaji ambaye mwisho wa siku naweza kujivunia pia part nyingine ya kazi ambayo naifanya, nataka niwe mkulima na mfugaji, 2017 nataka niuanze mwaka hivyo ukiacha muziki ambao nafanya.” Alisema Bushoke.

  Kitu kingine ambacho alifunguka Bushoke ni kuhusu kazi yake ya muziki na kudai kwamba hawezi kuiacha kazi yake hiyo kwasababu ni sehemu ya maisha yake.

  Unaweza kumsikiliza Bushoke akifunguka hayo na mengine mengi zaidi kwa kuplay hii video hapa chini.


   

  Dondosha comments


  Share this