Chege ameyaandika haya baada ya kuzushiwa kifo

  Share this

  Huko Facebook kuna mtandao mmoja umeripoti kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kiumeni Chege Chigunda amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari.

  Taarifa ambayo haina ukweli wowote bali imeandikwa tu na mtu ili kujitafutia viewers na vitu kama hivyo.

  Kupitia ukurasa wake wa instagram Chege amelaani vikali kitendo hicho na kuonyesha hali ya kushangazwa ni kwanini watu wamekuwa wakimuhusisha yeye na taarifa za kifo mara kwa mara.

  Kwenye post yake ya instagram Chege ameandika kwamba “Sidhani kama ni vema kuendelea kuombeana mabaya kila siku kwa kitu ambacho kina julikana na nilisha kitolea ufafanuzi kwamba hii pic ilikua ni movie tena zamani kabisa miaka zaidi ya minne ilopita kuendelea kutangaziana mabaya,Mungu anawaona na mbaya zaidi huwa analipa hapa hapa duniani,mimi sijapata ajali yoyote ndugu zangu,kusoma hamjui hata picha hamuoni?nimebadili nywele zangu muda sasa lkn napataje ajali na nywele hizo?sio vizuri,tuitumie mitandao yetu vizuri aisee,ndio maana mh magufuli aliwahi sema anatamani atokee malaika azime mitandao yote ni sababu ya watu wasio jua kwanini wapo kwenye mitandao”

  Pia Chege akaongeza “Mimi niko fresh kabisa lkn watu wenye haraka na wenye tamaa ya followers nawaomba msiwe wepesi wa kuandikiana mabaya,Mungu hapendi”

  Tunashauriwa kuwa waangalifu na taarifa zinazo postiwa mitandaoni hasa kwa ile mitandao ambayo sio rasmi.


   

  Dondosha comments


  Share this