Chege apingana na kauli ya “Kanumba ameondoka na Bongo Movie yake”

  Share this

  Ikiwa kitaani kuna tetesi kuwa tasnia ya filamu hapa nchini iliyumba na hatimaye kupotea kabisa kwenye ramani baada tu aliyekuwa muigizaji mkali Steven Kanumba kufariki Dunia.

  Kutoka Kiumeni Chege Chigunda amedai kuwa haungi mkono hata kidogo kauli hiyo ya Kanumba kuondoka na Bongo Movie yake kwasababu anaamini waasisi wa sanaa zote walikwisha fariki dunia ila sanaa zao bado zinaendelea kuwa na uhai mpaka leo hii.

  Chege amedai kuwa anaamini kuwa soko la movie Bongo linaonekana kushuka kwa hapa nchini kutokana na wenyewe wenye bongo movie yao kwa hivi sasa wanalenga soko la nje na kutaka kuipeleka sanaa yao mbali zaidi ndio maana kwa ndani linaonekana kuyumba kwa kiasi flani.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini kumsikiliza mwanzo mwisho Chege akifunguka kuhusiana na issue hiyo.

  Dondosha comments


  Share this