Diamond Platnumz awatolea MAPOVU wanao muandama Zari mitandaoni!

  Share this

  Baada ya Mama Tiffah, Zari Te Boss Lady kustream live kwenye page yake katika mtandao wa instagram akionekana anakula raha na mpenzi wake Diamond Platnumz wapo ambao wamekuwa na comments za tofauti katika kitendo hicho ukizingatia ni siku chache tu zimepiita tangu mrembo huyo afiwe na Mama yake mzazi.

  Diamond Platnumz ameamua kutowakalia kimya watu hao na kuwatupia madongo ya saizi yao huku akidai kwamba hii ni time ya kumpetipeti mpenzi wake huyo kutokana na matatizo ambayo amepitia siku chache zilizopita.

  Kupitia ukurasa  wake wa instagram Diamond Platnumz ameandika kuwa Kuna vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa Misiba ya watu…. Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehem tulivu apetiwepetiwe apate faraja!…sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo, Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia… Pambaneni na Mahusiano yenu…! Nina siku 5 za kumpetipeti… leo ndio kwanza Ya kwanza 😛

  Post ya Diamond

  Niachie comment yako kuhusu post hiyo ya Diamond Platnumz. yuko sahihi au amepuyanga yeye kama kioo cha jamii.

  Dondosha comments


  Share this