Dj Khaled atengeneza historia kwenye Apple Music

  Share this

  Kama alivyoahidi kwamba album yake ya “Grateful” lazima ichukue tuzo ya Grammy, matunda yameshaanza kuonekana kwa kutengeneza historia kupitia ngoma yake ya “Im The One”.

  Mashabiki wakiwa wanahamu kubwa ya kutaka kufahamu ujio wa album ya “Grateful” inaachiwa lini, Dj Khaled ameshaanza kuumiza na wimbo wake wa “im the One”, ambayo amemshirikisha Quavo, Lil wayne, Justin Bieber na Chance the rapper, Good Newz ni kwamba ngoma ya Dj Khaled imefanikiwa kutengeneza historia katika mtandao wa Apple Music kwa kuwa nyimbo ya kwanza kuwa streamed kimataifa kwa mara nyingi zaidi ndani ya wiki moja.

  Mbali na kutengeneza historia hiyo kwenye Apple Music, Dj Khaled ameingia kwenye chati za Bilboard Hot 100 akiwa namba moja na ngoma yake ya “Im The One”

  Dondosha comments


  Share this