Dogo Janja kujitapa kuvaa ni akili za utoto zinamsumbua-: Madee

  Share this

  Takriban wiki tatu sasa hitmaker wa ngoma ya Kidebe, Dogo Janja amekuwa akivimba katika mitandao ya kijamii akijitangaza kuwa yeye ndio msanii anaye ongoza kwa kupendeza kuliko wasanii wote Afrika mashariki.

  Kitu ambacho kimekuwa kikizua gumzo mara kwa mara katika mitandao ikiwemo na majibizano ya yeye na wasanii wenziye kama Nedy Music, Young Dee na wengineo.

  Madee ambaye ndiye msimamizi wa Dogo Janja amefunguka kuwa anachokifanya Dogo Janja kinatokana na umri wake.

  Akiongea kwenye XXL ya Clouds FM Madee amesema “Mimi bado naamini kuwa Dogo Janja bado ni mdogo, kwahiyo chochote anachokifanya nachukulia kama ni cha kitoto tu”

  Madee pia ameongeza kwa kusema kuwa “Sina uhakika kama mtu mzima anaweza kutoka hadharani na kujitangaza kuwa yeye ndiye anaongoza kwa kuvaa, kwahiyo kutokana na umri ambao yuko nao Janja, tumuache tu afanye kile ambacho anajiskia kufanya ilimradi tu havunji sheria za nchi.”


   

  Dondosha comments


  Share this