EXCLUSIVE: Sifanyi Muziki kwasababu ya Tuzo-: Alikiba

  Share this

  Ni maneno kibao yamekuwa yakiongelewa kitaani kutokana na ukimya wa mkali wa muziki wa Bongo fleva Alikiba katika kuachia ngoma, kitu ambacho mashabiki zake kuonekana kuwa na kiu isiyo na kifani ya ngoma mpya kutoka kwa mkali huyo.

  Katika Exclusive Interview ambayo Alikiba amefanya na PerfectoTV ameweka wazi mipango yake ya kuachia ngoma siku za hivi karibuni akidai kuwa kila kitu kimesha kamilika kuanzia audio mpaka video kilichobaki ni kuiachia tu.

  Kingine ambacho Perfect Crispin alihoji kwa Alikiba ni kuhusiana na mipango ya mkali huyo katika kutwaa tuzo kubwa kimataifa kutokana na muziki wake, ila King Kiba amefunguka kuwa yeye hafanyi muziki kwasababu ya tuzo, anachoangalia yeye ni kutoa ngoma kali ili mashabiki wake waipende, mambo ya tuzo yanakuja baadae.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini ili uweze kuitazama mwanzo mwisho interview hiyo ambayo Alikiba amefunguka mengi kuhusiana na muziki, biashara na hata maisha yake binafsi.


   

  Dondosha comments


  Share this