FREESTYLE ALIZOZIDONDOSHA EMINEM KWENYE CYPHER YA BET HIPHOP AWARDS 2017 NI ZAIDI YA BOMU

  Share this

  Wakati tukiwa na kimuye muye cha kutaka kufahamu ujio wa Album ya Eminem ambayo inatarajiwa kutoka Novemba mwaka huu, Usiku wa tuzo za BET HIPHOP AWARDS jana Jumanne, Eminem alidondosha Freestyle moja hivi ambayo ni kama bomu la Nyuklia kwa Donald Trump, wakati Bomu hilo la Freestyle likiwa linateketeza kila kitu, Wasanii kibao wa HipHop wametoa shangwe zao kwa Eminem.

  Image result for EMINEM BET HIP HOP AWARDS 2017

  Wengi tunafahamu uwezo wa Eminem anapokuwa anaachia vinu vyake huwa hakwepeshi kila anapolenga target yake, Sasa kupitia Cypher ambayo ilifanywa na BET HIPHOP AWARDS 2017, rapper kutoka Detroit, Eminem aliamua kudondosha bomu lake mpaka kwa Donald Trump ambalo lilikuwa na dakika nne za kulitegua, Moja ya madongo ambayo alimdondoshea Donald Trump ni kuhusu maswala yaliyokuwa yanendelea ya NFL, majanga ya Puerto Rico pamoja na ukuta ambao Trump amepanga kuujenga huko Mexico.

  Image result for EMINEM BET HIP HOP AWARDS 2017

  Freestyle hiyo imewafanya wasanii kibao kama J Cole, Snoop Dogg, TPain, Mack Maine na wengine kibao wameonyesha kuiunga mkono Freestyle hiyo, Kasoro T Pain ameomba tu watu wakae makini kumlinda Eminem.

  Dondosha comments


  Share this