FREESTYLE YA EMINEM KUHUSU DONALD TRUMP, IMECHAFUA HALI YA HEWA TWITTER NA KUWEKA REKODI

  Share this

  Mitandao ya Kijamii bado hali ya hewa yake imechafuka ile mbaya baada ya Eminem kuachia Freestyle yake ambayo amemdiss Rais wa Marekani Donald Trump kupitia BET HIPHOP AWARDS 2017 CYPHER iliyofanyika usiku wa Jumanne, Video hiyo imetengeneza Tweet takribani Milioni 2, ambapo sio hali ya kawaida.

  Rapper Eminem anatufanya mashabiki zake tukae kwa hamu kungoja hiyo Album yake inayotarajiwa kutoka hivi karibuni Novemba 17 mwaka huu, Sasa unaambiwa hiyo Freestyle ya Eminem ambayo ameipiga akapela kwa kumdiss Donald Trump imetengeneza historia kwa Video hiyo kuwa Tweeted mara Milioni 2 katika mtandao wa Twitter.

  Freestyle hiyo bado inatengeneza majadiliano mengi kwa watumiaji wa Twitter pamoja na mashabiki, Kama ulipata nafasi ya kusikiliza hiyo Freestyle, Eminem alimchana Donald Trump kwa kutumia muda mwingi katika kutumia mtandao wake wa Twitter na kusababisha kutojitoa kwa wananchi wake. Mashabiki bado wamekaa kusubiri kuona Rais Donald Trump atajibu nini.

   

  Dondosha comments


  Share this