Haikuwa rahisi kufunga ndoa na Grace-: Professor Jay

  Share this

  Moja kakti ya story zilizochukua nafasi kubwa sana weekend iliyopita kila kona ni kuhusiana na mkongwe wa muziki wa Hiphop nchini ambaye pia hivi sasa ni Mbunge wa jimbo la Mikumi Professor Jay kufunga Ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Grace Mgonja.

  Unaambiwa Professor Jay alidumu katika mahusiano ya uchumba na mpenzi wake huyo kwa takriban miaka 13 hadi kufikia kufunga ndoa, safari ndefu iliyokumbwa na misukosuko ya kila aina kama ilivyo kawaida katika mahusiano ya kawaida.

  Professor Jay ametusanua kwamba ilifika time wakatengana kabisa katika mahusiano na kila mmoja akaendelea na mahusiano mapya ila mwisho wa siku walikuja kurudiana kwasababu kila mmoja aliamiini kuwa mwenza wake ndio chaguo sahihi kwake.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini uweze kumsikiliza Professor jay akisimulia japo kwa ufupi historia yake na misukosuko ambayo wamepitia na mpenzi wake huyo.


   

  Dondosha comments


  Share this