Haya sasa kwa wale watoto wakiume wasiopenda kujituma, Shamsa Ford ana ujumbe

  Share this

  Mrembo wetu kutoka kwenye kiwanda cha Filamu Bongo, Shamsa Ford aamua kuwapa msaada wa maneno vijana wa Kibongo ili kujituma.

  Sio Jambo baya kama mtu akiamua kuongea ukweli kwa ajili ya kukusaidia na nio kitu ambacho kimempelekea Shamsa kutumia kurasa yake ya Instagram kuandika ujumbe kwa vijana ambao hawapendi kujituma ila wanachosubiri ni kulelewa tu na majimama.

  “kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii. usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofcn wakati elimu yako ni darasa la pili. mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha.Sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie RIZIKI .Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi .ukishajiona una sura nzuri basi na wewe Eti unadanga kwa jimama lenye pesa 😃😃. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa. Hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?Mara VIBENTEN,VIPANYABUKU,VICHURA,VITORM AND JERRY ….Daaa inauma ..”

  Dondosha comments


  Share this