Hii ndio sababu ya Video ya Ngoma ya Young Killer kukaa kwenye Youtube Chanel ya Harmonize

  Share this

  Moja kati ya maswali ambayo yamekuwa yakikosa majibu kwenye vichwa vya watu wengi ni pamoja na hili la ngoma za wasanii ambao wamekuwa wakiwashirikisha wasanii kutoka WCB, video za ngoma hizo kuwa zinakaa kwenye Youtube Chanel za wasanii hao wa WCB na sio wamiliki wa ngoma hizo kama ilivyo kawaida.

  Tukianza na Inde ya Prince Dully Sykes aliyomshirikisha Harmonize, tukija kwa Stereo na ngoma yake ya Mpe Habari aliyomshirikisha Rich Mavoko na hata hii ya Unaionaje ya Young Killer ambayo imedropishwa wiki iliyopita amemshirikisha Harmonize.

  Perfect255 imeamua kumtafuta Young Killer na kupiga naye story kuwa imekuaje kiupande wake video ya ngoma yake kukaa kwenye Youtube Chanel ya Harmonize ikiwa inafahamika fika kuwa mtonyo wa Youtube ndio kitu ambacho kinatolewa macho na wasanii weng kwa sasa.

  Young Killer ameiambia Perfect255 kuwa kwa upande wake hajawahi kunufaika kwa chochote kutoka kwenye Youtube Chanel yake na ndio sababu ya video yake hiyo kukaa kwenye chanel ya Harmonize angalau iweze kupata nguvu na kuingiza chochote kitu katika suala zima la mtonyo.

  “Kiukweli Youtube imekuwa ni chanzo kikubwa cha kuwaingizia watu hela kwa kiasi kikubwa sana, lakini mimi binafsi sijawahi kunufaika chochote kupitia Youtube.” Alisema Young Killer.

  Pia Young Killer aliongeza kuwa video ya “Unaionaje” ni video kubwa iliyogharimu pesa nyingi zaidi kwahiyo inahitaji angalau ipate chochote kile ili watu waweze kunufaika kwa kile ambacho wamekifanya, ukizingatia chanel ya Harmonize ni chanel iliyosajiliwa na inaingiza pesa nyingi.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini uweze kumsikiliza Young Killer akifunguka mwanzo hadi mwisho kuhusiana na issue hiyo.


   

  Dondosha comments


  Share this