Hii ndio Skendo ya Wolper iliyomuumiza zaidi Harmonize kipindi cha Mahusiano yao

  Share this

  Hakuna asiyefahamu kwamba miezi michache iliyopita Entertainment Industry hapa Bongo ilikuwa ikiambatana na couple ya mastaa wawili kutoka katika nyanja tofauti tofauti katika wigo wa Entertainment.

  Mmoja kutoka Bongo Flevani ambaye ni Harmonize wa WCB na kutoka Bongo Movie ni mrembo Jacqueline Wolper ambao kwa hivi sasa kila mmoja anaendelea na mahusiano mapya baada ya kuvunjika kwa uhusiano wao.

  Ikiwa inajulikana mastaa hao ni watu wa skendo kila kukicha, jana July 17 Harmonize ameshare na sisi story kuhusu skendo ambayo ilimuumiza zaidi katika mahusiano yake na Wolper.

  Kupitia Amplifaya ya Clouds fm Harmonize ametusanua kuwa skendo ya Jacqueline Wolper kurecordiwa video akiwa mtupu na aliyekuwa mpenzi wake kipindi cha nyuma ni kitu ambaccho kilimuumiza sana na kumfanya afikirie itakuwa vipi endapo video hiyo ikivuja.

  Katika hali ya kimapenzi Harmonize amedai kuwa alikuwa akijipa moyo juu ya hilo ukizingatia mpenzi wake huyo sio mtu wa kwanza kutokewa na jambo kama hilo, akitolea mfano mastaa wakubwa Duniani kama Kim Kardashian, Ammber Rose ni watu ambao wamewahi kukumbwa na skendo kama hizo na maisha yakaendelea.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini ili uweze kumsikiliza Harmonize akizungumzia kiundani suala hilo.


   

  Dondosha comments


  Share this