Hiki ndicho kitu ambacho Lulu Diva anajutia kukifanya katika maisha yake

  Share this

  Katika hali ya kawaida tu maishani yapo mambo ambayo kila mmoja anafanya na baadae mtu anakuja kujutia kile ambacho alikifanya kwa kujua ama kutojua.

  Kwa upande wa msanii Lulu Diva hitmaker wa ngoma ya Utamu wengi tulianza kumfahamu mrembo huyo baada ya kutokea kwenye video nyingi za muziki hapa Bongo {Video Vixen}, kitu ambacho binafsi anakijutia kukifanya japo kuwa anadai alikifanya kwa malengo ila sio kitu ambacho alikuwa akikipenda.

  Lulu Diva anadai kuwa alifanya u-video vixrn ili kupata urahisi wa kuwa na chanels za yeye kuingia kwenye muziki jambo ambalo alikuwa analipenda ila akawa anashindwa pakuanzia na kuamua kuwa video vixen kutokana na kuwa ni kitu ambacho kitamuweka karibu na wasanii na kuweza kumpa njia za kupita.

  Lulu Diva anadai kuwa kutokana na jinsi ambavyo wamejiweka ma video vixen wa Tanzania na hata ambavyo jamii inawachukulia ni moja kati ya vitu vikubwa ambavyo vilikuwa vikimfanya aichukie kazi hiyo ikiwa na pia hata familia yake ilikuwa haipendelei kumuona kwa upande huo.

  Yapo mengi sana ambayo ameyaongea Lulu Diva, unaweza kumsikiliza mwanzo mpaka mwisho kwa kubonyeza play kwenye video hii hapa chini.


   

  Dondosha comments


  Share this