HILI NI PIGO KUBWA KWA WAONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI NCHINI TANZANIA

  Share this

  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imepiga marufuku urushwaji angani wa vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kupata kibali maalum cha mamlaka hiyo.

  Related image

   

  Taarifa iliyotolewa kwa umma na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imeeleza kuwa kuanzia sasa kwa taasisi au mtu binafsi kufanya anayetaka kununua au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na kibali kutoka katika  Mamlaka hiyo.

  Amesema uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo kwa hiyo basi ametoa tamko kuwa si ruhusa kurusha kifaa hiko pasipo kuwa na kibali maalumu kutoka mahala husika.

  Kwa sasa hapa nchini drone zimekuwa zikitumika kwa ajili ya kupiga picha za angani maeneo ya mashamba makubwa, mkusanyiko mkubwa wa watu. Pia zimekuwa zikitumika mara nyingi katika kuandaa video za muziki.

  Related image

   

  Dondosha comments


  Share this