Hizi ndizo lebo anazozitamani Harmonize kufanya nazo kazi endapo akitemwa WCB

  Share this

  Ukiizungumzia WCB unazungumzia moja kati ya lebo kubwa sana Barani Afrika, ikiwa Harmonize ndio mmoja kati ya wana wanaokinukisha katika lebo hiyo.

  Harmonize amefunguka kuwa endapo kibarua kikiota nyasi kwenye lebo yake ya WCB zipo lebo ambazo yeye kama yeye anazitamani kufanya nazo kazi.

  Harmonize amezitaja Young Money na Roc Nation kama ndio lebo ambazo anatamani kufanya nazo kazi akidai kwamba WCB ni lebo kubwa Africa kwahiyo endapo akiondoka hapo hatahitaji tena kurudi nyuma na hivyo ataenda worldwide.

  “Ikitokea kufanya kazi na lebo nyingine, lebo yoyote tunaweza kufanya kazi ila me ninawish Roc Nation au Young Money kwasababu siwezi kutoka WCB nikaenda lebo nyingine ya kawaida kwasababu ukizungumzia WCB unazungumzia lebo kubwa Africa kwahiyo nikitoka Africa natamani kwenda worldwide.” Alisema Harmonize

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini ili uweze kumsikiliza kiurefu Harmonize akifunguka juu ya suala hilo.

  Dondosha comments


  Share this