Huenda Dogo Janja alitabiri kuachana kwa Harmonize na Wolper

  Share this

  Kabla ya hii “Ukivaaje Unapendeza” Dogo Janja alikuwa anahit na ngoma yake ya Kidebe, kama uliisikiliza vizuri Kidebe kuna line inasema “Mapenzi ya sinema ni ya harmonize na Wolper“.

  Siku chache zilizopita Wolper na Harmonize walimake headlines baada ya kutangaza rasmi kwenye media kuwa hawapo tena katika mahusiano ya kimapenzi, kitu ambacho kiasi flani kinaleta picha na mistari ya Dogo Janja.

  Janja amepiga story na Perfect55 aliona nini kwenye couple hiyo hadi kufikia hatua ya kuiweka line hiyo kwenye ngoma yake na hatimaye leo kimetokea kweli.

  “Ukishakuwa na mpenzi star hiyo ni filamu tayari, maisha yenu ni filamu, watu wanafuatilia maisha yenu kama filamu. Kitu kingine mapenzi yao yalivyokuwa yanaanza watu walikuwa wanachukulia kama drama ila mwisho wa siku wakaja kuona kuwa wako serious” Alisema Dogo Janja.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini uweze kumsikiliza Dongo Janja akifunguka mwanzo mpaka mwisho kuhusiana na issue hiyo.


   

  Dondosha comments


  Share this