‘Im The One’ ya Dj Khaled ni vumbi tuuu

  Share this

  Hata kabla ya ujio wa “Grateful” matunda yake yashaanza kuonekana kupitia ngoma ya “Im The One”.

  Baada ya kutengeneza historia katika mtandao wa kustream ngoma wa Apple Music, na kutengeneza rekodi kwa kushika nafasi ya kwanza katika chati ya Billboard hot 100 na ngoma yake ya “Im The One”, Dj Khaled ameibuka upya kwa ngoma hiyo kuwa certified gold kwa kuuza kopi takribani 500,000.

  Ngoma hiyo imebeba vyuma kama Quavo, Lil wayne, Justin Bieber, na Chance The Rapper, ambacho kinanogesha zaidi ni kwamba nyimbo hiyo inawiki mbili tangu itoke, kupitia kurasa yake ya Instagram Dj Khaled aliandika kwa kusema kwamba “Bless up fan luv !! ANOTHER ONE #IMTHEONE OFFICIALLY #GOLD  And the rec only been out for 2 weeks .. WOW BE PLATINUM any day now @wethebestmusic @epicrecords @rocnation FAN LUV THANK YOU IM SO #GRATEFUL”

  Dondosha comments


  Share this