INAWEZEKANA DJ KHALED KUWA BOSS MPYA BAADA YA ANTONIO MARQUIS KUACHIA NAFASI EPIC RECORDS

Share this

Dj Khaled anadaiwa kuitaka nafasi iliyoachwa wazi na Antonio Marquis maarufu kama L.A. Reid katika lebo ya Epic Records.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu cha rapper huyo kimeiambia Page Six kuwa Khaled anaitaka nafasi ya uwenyekiti wa lebo hiyo ambayo imekuwa wazi kwa takribsni wiki mbili sasa.

He was petitioning to get that job. He’s like, ‘I make more happen than anyone in the game, why would I not be considered to run the label?,” kimesema chanzo hiko.

Mpaka sasa bado uongozi wa Sony Music ambao ndio wamiliki wa Epic Records hawajazungumza chochote kuhusu kujiuzulu kwa Reid. Hata hivyo kuna baadhi ya taarifa ambazo siyo rasmi zinadai kuwa bosi huyo amejiuzulu kutokana na kashfa ya kumdhalilisha mmoja wa wafanyakazi wa kike wa lebo hiyo.

Dondosha comments


Share this