ISHU YA NELLY YA UBAKAJI IMESHIKA PETROLI

  Share this

  Ishu ya Nelly kuhusu tuhuma za Ubakaji zinazidi kupamba moto, Huyo Mwanamke ambaye amemfungulia Nelly mashitaka ameibuka na kudai kwamba anatishiwa Amani pamoja na kunyanyaswa na Msanii huyo.

  Image result for nelly

  Kama utakumbuka Hivi karibuni Nelly alikumbana na kesi ya Ubakaji huko jijini Washington kwenye Bus Tour lake, Ambapo yeye mwenyewe alitumia kurasa yake ya Twitter kupinga ishu hiyo na kusema kwamba ni kutaka kumchafulia jina, hata Mwanasheria wa Nelly nae alifunguka kuhusu hilo na kudai kwamba hizo taarifa anazotoa mwanamke huyo ni za Uongo.

  Moto kama umedondoka kwenye nyasi kavu, Mwanasheria anayesimamia ishu ya huyo Mwanamke ambaye analalamika kubakwa, ameibuka na kudai kwamba Nelly anamtishia Amani pamoja na kumnyanyasa.

  Related image

  Ishu hiyo inazidi kukua ambapo mwisho wa siku, Mwanasheria wa Mwanamke huyo, Koehler, anadai kwamba lazima haki ipatikane kwa kosa ambalo amelifanya Nelly.

  Related image

  Dondosha comments


  Share this