Jifunze kitu hapa kutoka kwa Kevin Hart

  Share this

  Moyo wa kuomba kwa ajili ya kuwa na mafanikio na maisha mazuri, naweza nikasema kila mtu kabalikiwa na hiko kitu, ila moyo wa kutoa kwa watu wasiojiweza, hii ninaweza kuipa nafasi ndogo sana kwa maisha ya Sasa.

  Ila hiyo sio kesi kwa  mchekeshaji nguli Duniani mwenye mafanikio makubwa katika tasnia ya filamu mpaka Stand Up Comedy, namzungumzia Kevin Hart, mbali na kuwa na moyo wa ustaa, mchekeshaji Kevin Hart ametuonyesha moyo wa kusaidia wasiojiweza, Katika pita pita zake kitaani, Kevin Hart alikutana na Mama Omba Omba ambae alimpatia dola za kimarekani 400 ambazo tukizipeleka katika pesa zetu za madafu ni sawa na mtonyo kama wa laki nane hivi.

  Sio mbaya najua hata wasanii wetu wabongo wamejaaliwa mioyo na wanaweza wakijifunza vingi pia katika kuwa na moyo wa kusaidia wengine.

  Dondosha comments


  Share this