KAMA ULIKUWA HUFAHAMU BASI HIKI NDIO CHANZO CHA KUANZISHWA KWA MTANDAO MPYA WA DAXOGRAM

  Share this

  Baada ya kutokea tatizo katika Mtandao wa Instagram ambalo linatajwa kupelekea akaunti ya Selena Gomez kuweza kudukuliwa, Wadukuzi hao wameungana pamoja na kutengeneza Website yenye uwezo wa kuuza akaunti za watu ambao wako Verified kwenye mtandao wa Instagram.

  Image result for instagram

  Dosari hiyo kutoka Instagram imesababisha namba za simu, Anuani na Nywila(Password) za watu maarufu kuweza kutambulika na Wadukuzi, japo mtandao huo umekanusha kuwa wadukuzi hao hawajafanikiwa na chochote.

  Website iliyofunguliwa na Wadukuzi hao wameipa jina la DOXAGRAM, ambapo kwenye website hiyo kuna huduma ya kutafuta akaunti ya mtu maarufu yeyote yule kwenye Instagram na ili uweze kugaiwa taarifa kuhusu mtu huyo basi Website hiyo itakuitaji kulipia dola 10 kwa kila akaunti moja.

  Image result for selena gomez

  Mpaka sasa INSTAGRAM hawajaongea chochote kuhusu Ishu hiyo ya kuwepo na Website yenye uwezo huo wa kutoa taarifa za watumiaji wake,  ila umetoa ushauri kwa watumiaji wa mitandao  wawe makini na Website za aina hizo kutokana na nyingi huwa na virusi ambavyo vinaweza kuharibu kifaa chako au kuiba taarifa zako.

  Dondosha comments


  Share this