Kingine usichotakiwa kukikosa kutoka kwa Nikki wa Pili

  Share this

  Imezoeleka kuwa mkali kutoka Chugani chini ya kampuni ya Weusi Nikki wa Pili sio mtu wa kuonekana kwenye vichupa mara kwa mara, yeye mwenyewe analitambua hilo ndio maana time hii ameamua kufanya kama kukomoa hivi.

  Nikki wa Pili amebonga na mashabiki zake na kuwasanua kuwa wategemee video mbili kwa mpigo ambazo anatarajia kuzidropisha siku yoyote kuanzia leo hii.

  Kupitia ukurasa wake wa Twitter ndio sehemu ambayo Nikki alichukua muda wake na kuweza kudondosha habari hiyo, huku tweet yake ikisomeka kama “Kile kilio kuwa sitoi video sasa video mbili zinadondoka siku yoyote #genius kababaa, madenge niki kiminyio.”

  Dondosha comments


  Share this