Kipo ambacho Babu Tale amekiona kwa African Princess “Nandy”

  Share this

  Ukizungumzia wadada ambao wanafanya poa kwenye game ya music kwasasa hakika huwezi kuacha kumtaja mwanadada Nandy. Kutokana na  hit baada ya hit anazotengeneza mrembo huyo kutoka Tanzania House of Tallent (THT).

  Meneja wa Diamond Platnumz na Tiptop Connection Hamisi Taletale almaarufu kama Babu Tale kipo ambacho amekiona kwa mrembo huyo na kuamua kutoficha hisia zake.

  Kupitia ukurasa wake wa instagram Babu Tale ameandika kuwa “Naona manager @saleh_gadau binti ameweka. Kaza mrembo nakuona mbali sana @officialnandy”

  Naona manager @saleh_gadau binti ameweka. Kaza mrembo nakuona mbali sana @officialnandy

  A post shared by Hamisi Taletale (@babutale) on

  Bila kupepesa maneno ni kutokana na juhudi ambazo zinaonyeshwa na mwanadada Nandy ndio maana Babu Tale ameweza kumtabiria makubwa mrembo huyo.

  Ikumbukwe kuwa Nandy ni mmoja kati ya Watanzania ambao wanaipeperusha bendera ya nchi kwenye Coke Studio ya mwaka huu wa 2017 Nairobi Kenya.

  Dondosha comments


  Share this