Kuomba msaada kumemtokea puani Nicki Minaj

  Share this

  Rapper Nicki Minaj ameamua kujiunga kwenye ulimwengu wa mtandao wa Snapchat, ila Bad newz ni kwamba Nicki Minaj anahitaji msaada wako jinsi ya kutmia mtandao huo.

  Kupitia kurasa yake ya Instagram, Nicki Minaj aliamua kushare ujumbe na mashabiki wake kwamba kajiunga na mtandao wa Snapchat, mbali na kujiunga Nicki aliamua kujibu comments za mashabiki kuelekezwa jinsi gani anaweza akutumia mtandao huo ambao ndio amefungua akaunti yake mpya, Balaa linaanza ndani ya comments Nicki anaanza kuwauliza mashabiki jinsi gani anaweza kufanya akaunti yake ikawa public huku akiomba alekezwe jinsi ya kuweza kuona watu waliomfollow.

  Mbaya Zaidi ikampelekea sasa kushindwa kuweka setting zake vizuri na kujikuta kila muda mashabiki wake wanampigia simu na kumtumia Meseji kila baada ya sekunde 30,  alichoamua kukifanya ni kwamba ameamua kuilog off akaunti yake kwanza ili akawekewe setting  kwa ajili ya kuutumia mtandao huo wa Snapchat vizuri kutokana na kwamba inakuwa rahisi mashabiki zake kupiga simu, kutuma sms tena kwa fujo.

  Omgggggggg why y'all doin this to me? 😩 Candice can't even help me. They gotta call Snapchat now 🙃

  A post shared by Barbie® (@nickiminaj) on

  Dondosha comments


  Share this