Madee aamua kuongea ukweli kwa wasanii wa aina hii…

  Share this

  Muziki wa Bongo fleva umezidi kuwa tishio kila siku kwa wasanii ambao hawajaachia ngoma mpaka kumfanya Madee kushuka ujumbe kwa wasanii wenzake ambao wanahisi wanabaniwa kwenye game ya Bongo.

  Kama ni mfuatiliaji mzuri wa radio mbali mbali hapa Bongo, utagundua kitu kwamba wasanii wa Bongo kama wameamka kwa kuachia mawe juu mawe kwa mashabiki zao, mfano kama Diamond, Young Killer, Weusi, Timbulo, Chege, Rich Mavoko na wengine kibao kama wanachafua hali ya hewa, Sasa kupitia akaunti ya twitter ya Madee aliamua kuandika ujumbe kwa wasanii wenzake kuwaambia kama hawana ubunifu katika kazi zao wasilalamike kubaniwa katika vyombo vya habari.

  Kupitia kurasa yake ya Twitter Madee aliandika hivi, “Radio na Tv zinazidiwa na utitiri wa nyimbo mpya zinazotoka kila siku!so kama msanii sio mbunifu usilalamike unabaniwa”

  Dondosha comments


  Share this