Madee ajibu tuhuma za kuandikiwa nyimbo na Rayvanny

  Share this

  Kitaani kulikuwa na tetesi kumuhusu mkali wa muziki kutoka Manzese Madee zikidai kwamba mkali huyo hivi sasa hafanyi poa kwenye game kutokana na kuwa alikuwa amezoea kuandikiwa ngoma na Rayvanny ambaye kwasasa yuko chini ya lebo ya WCB.

  Leo Madee ameamua kuzitolea uvivu story hizo na kudai kwamba yeye yuko kwenye game kwa miaka 16 sasa ikiwa huyo Rayvanny ndio kwanza ana miaka 3.

  Madee amedai ameanza kutengeneza hits tangu mwaka 2001 kipindi ambacho hata huyo Rayvanny hajajua muziki ataanza lini, inakuwa vipi leo hii isemekane kwamba yeye anamtegemea Rayvanny.

  “Ray anayo nafasi ya kuniandikia kama mimi nitaamua, lakini sio mimi kumtegemea Ray kuniandikia ngoma. Kama hicho nakitaka nitakifanya kwasababu sio kwamba ni kosa na wala sioni tatizo, ila suala la mimi kuandikiwa ngoma zangu na Ray hivyo ni vity viwili tofauti.” Alisema Madee

  Kwa msisitizo Madee amefunguka kuwa ameanza kuandika ngoma miaka 16 iliyopita na pia amekanusha vikali suala na kuwahi kuandikiwa ngoma na Rayvanny.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini uweze kumsikiliza Madee akifunguka juu ya mchongo huo.


   

  Dondosha comments


  Share this