Mr Nice amaliza Utata huu kuhusu video ya Harmonize “Sina”

  Share this

  Ikiwa vichwa vya Habari kubwa za siku kwenye vyanzo tofauti tofauti vya Habari nchini Tanzania vimesehei jina la Mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Mr Nice kwa mara nyingine tena baada ya muda mrefu kupita.

  Ikiwa ni baada ya mkali huyo kutokea kwenye video ya wimbo mpya wa Harmonize unaokwenda kwa jina la Sina. Wimbo ambao unamzungumzia mtu flani ambaye alipata mabovu kipindi cha nyuma kisha kuyatumia kwa fujo na mwisho wa siku akaja fulia. Kitu ambacho Mr Nice amebeba maana halisi ya ujumbe wa wimbo katika video hiyo.

  Maswali ni mengi kitaaani kuhusiana na video hiyo, ikiwa wengine wanadai kwamba labda pengine Mr Nice amefanya kwa bure tu katika maana ya kumsaidia mdogo wake katika game huku wengine wakidai kwamba ni mpunga mrefu kinoma ambao ameuvuta Mr Nice katika kushoot video hiyo.

  Katika kipindi cha D’Weekend Chat Show cha Clouds TV (Shilawadu) Mr Nice amemaliza utata huo kwa kuweka wazi kwamba amelipwa kufanya video hiyo na wala hakuna kingine ambacho kina endelea baina yao baada ya kufanyika kwa video hiyo.

  Mr Nice amekataa kukiweka wazi kiasi ambacho amelipwa na Harmonize ili kufanya video hiyo ispokuwa amesisitiza tu kwamba pale alikuwepo kikazi na si vinginevyo.

  Dondosha comments


  Share this