Mtazamo wa B Dozen kuhusu kauli ya Nikki wa Pili kulalamikia Media

  Share this

  Moja kati ya mambo ambayo yalitrend kinoma siku ya jana kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na post ya Nikki wa Pili katika mtandao wa instagram akizungumzia vitendo vya baadhi ya media hapa nchini kuhoji wasanii wa ndani pale ambapo wanaamua kutoa ngoma kwa mfululizo.

  Post ya Nikki

  Caption ya Nikki wa Pili ilisomeka kama Drake, wizi kid, davido, dj khalid, major lazer naskia kwenye media mbali mbali hapa nyumbani wakisifiwa kuwa wanakimbiza kwakuwa wana hits nyingi kwa wakati mmoja
  Lakini kama mmsemaji wa weusi nimekuwa nikihojiwa na media kibao kuwa kwanini mmetowa hits zenu haraka haraka hamuoni mnauwa track zenu wenyewe????? Alafu hapo hapo wanakuuliza nin kifanyike ili muzik wa tz ukuwe???? Kazi itakuwaje kama wafanyakazi wakifanya kazi wanaambiwa wanauwa kazi???

  Leo kwenye XXL ya Clouds fm moja kati ya mambo yaliyozungumziwa kiundani ni pamoja na post hiyo ya Nikki wa Pili na kila mmoja kutoa ufafanuzi kwa ambavyo yeye ameielewa.

  B Dozen amefunguka kuwa anaamini Weusi wameridhika ndio maana ngoma zao hazifiki sehemu ambayo wanataka, moja kati ya sababu ambazo Dozen amezitoa ni kutokuwa na video kwa ngoma nyingi za Weusi, kitu ambacho pengine kinachangia kwa ngoma kutokuwa na uhai mrefu.

  Sababu nyingine ambayo Dozen ameitoa ni tittle za ngoma nyingi za Weusi kwasasa kucheza na trend ambayo ipo nchini kwa wakati huo, ukiangalia ngoma kama Madaraka ya Kulevya ilivyotoka wakati ule mambo ya kisiasa yamechukua nafasi hapa nchini, na hata Naliamsha Dude ikiwa ni neno ambalo lilitrend kwa wakati huo baada ya kuongelewa na Askofu Gwajima.

  Kiurefu zaidi msikiliza Twangala Twizzy akifafanua kwa muono wake kauli hiyo ya Nikki wa Pili. Bonyeza play kwenye video hii hapa chini kusikiliza.


   

  Dondosha comments


  Share this