MUME WA ZAMANI WA ZARI AFARIKI DUNIA KWA MARADHI YA MOYO

  Share this

  Aliyekuwa mume wa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mzazi mwenzake ‘Ivan Ssemwanga’ amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda kiasi cha kulazwa katika hospitali ya Steve Biko Academic mjini Pretoria nchini Afrika Kusini.

   

  Image result for zari na ivan

  Ivan alipimwa na kuonekana kuwa na kiharusi hata kukosa fahamu kwa muda wa siku 11 ambapo taarifa za awali zilisema kuwa alisumbuliwa na maradhi ya Shambulio la Moyo (Coronary Artery Disease). Wiki iliyopita alikimbizwa hospitali mara tu baada ya kupoteza fahamu hali ambayo ilionekana kumnyima raha Zari hata kutuma ujumbe katika mtandao wa SnapChat na Instagram kuwa yuko katika kipindi kigumu hivyo wamuombee Ivan kutokana na hali aliyokuwa nayo kiafya kuonekana kuwa mbaya.

  Kupitia ukurasa wa Instagram Zari ametuma ujumbe wa taarifa za kufariki kwa mzazi mwenzake huyo,Hata hivyo Zari na Ivan amefanikiwa kupata watoto watatu ambao Zari anaishi nao Afrika Kusini.

   

  https://www.instagram.com/p/BUfw89cjI0K/embed/captioned/?cr=1&v=7#%7B%22ci%22%3A0%2C%22os%22%3A12119.76%7D

   

  Dondosha comments


  Share this