Mwaka huu nimekosa BET, mwakani lazima niingie-: Diamond Platnumz

  Share this

  Wiki iliyopita zilitangazwa niminations za tuzo za kituo cha televisheni cha BET cha nchini Marekani, tuzo ambazo mwaka jana Tanzania iliwakilishwa na Diamond Platnumz, lakini mwaka huu mambo yamekwenda hovyo kwa mkali huyo na kujikuta akipita kavu kwenye tuzo hizo.

  Kupitia XXL ya Clouds fm hapo jana Diamond Platnumz amedai kwamba mwaka huu wamefanya kupokezana na wasanii wa Afrika magharibi, akimtolea mfano Davido ambaye mwaka jana hakutokea kwenye tuzo hizo lakini mwaka huu amepata nafasi ya kuwania tuzo hizo.

  Pia Diamond ametoa ahadi kuwa mwaka huu amejipanga kufumua madude ili kuhakikisha mwakani jina lake linatokea kwenye kuwania tuzo hizo.

  “Nasubiri mwezi wa Ramadhani uishe nianze kufumua mifululu ili tukutane mwakani.” Alisema Diamond Platnumz

  Full interview nimekuwekea kwenye video hii hapa chini, bonyeza play uweze kuisikiliza mwanzo mpaka mwisho.


   

  Dondosha comments


  Share this