Nay wa Mitego aweka wazi sababu za Album yake na Diamond kuchelewa

  Share this

  Kama unakumbukumbu nzuri utakumbuka kwamba Nay wa Mitego na Diamond Platnumz walishawahi kutusanua kuwa wanatarajia kuja na projects kibao za pamoja ikiwemo mambo ya album na vitu kama hivyo.

  Lakini ni muda mrefu umepita sasa na hatujaona mpango wa album wala single ya pamoja kama walivyodai hapo awali.

  Perfect255 imeona sio kesi kama itamtafuta Nay wa Mitego na kupiga naye story kuhusiana na mchongo huo umekaa vipi, kimya kutawala na vitu kama hizo.

  “Ni katika kuangalia mazingira mazuri ya kulinda kile ambacho tutakuwa tumekifanya, na kama tunavyojua siku hizi watu ambao wanaharibu kazi zetu ama watu ambao wanauza kazi zetu kiholela wamekuwa ni wengi, nimeona watu wawili,  watatu hapa wametoa album lakini naona imekuwa kama wametoa sadaka, kwasababu tayari kila mtu anayo na sina imani kama wameingiza hata milioni, hatukuwa tayari kufanya biashara ya hivyo.” Alisema Nay wa Mitego.

  Nay wa Mitego aliendelea kusisitiza kuwa hilo ni wazo ambalo lilikuwepo baina yake yeye na Diamond na kudai kwamba muda ukifika watalitendea kazi wazo hilo.


  • #Freestyle: Cheki Rayvanny alivyoumiza kwenye beat ya “Up in the Air” ya Rosa Ree

  Dondosha comments


  Share this