Nilichokilenga kimefanikiwa-: Benpol

  Share this

  Siku chache zilizopita moja kati ya story kubwa mitandaoni ilikuwa ni kuhusu picha alizokuwa akizipost msanii wa Bongo Fleva Benpol, picha ambazo zilikuwa zikimuonyesha akiwa mtupu na amefungwa kamba kama vile ametekwa.

  Picha ambazo zilizua gumzo kubwa sana na kila mtu kuweza kuzungumza yakwake kadri alivyozitazama picha hizo kwa jicho lake ikiwa wengi hawakuwa na mapokeo mazuri na picha hizo na kumshutumu Benpol kwa ambacho amekifanya.

  Leo kwenye Jahazi la Clouds fm Benpol amefunguka na kudai kuwa kile ambacho alikilenga katika kupiga picha hizo kimefanikiwa kwa asilimia 100%.

  Benpol amefunguka kuwa picha zile zina maudhui kulingana na wimbo wake anaotarajia kuutoa masaa machache yanayokuja, kulingana na kazi yake ijayo inahusisha mambo ya utekwaji ndio maana aliamua kufanya kitu kama hicho.

  Tumia sekunde chache kumsikiliza Benpol akifunguka juu ya jambo hilo kwa kubonyeza play kwenye video hizi fupi.


   

  Dondosha comments


  Share this