Pambano la ngumi kati ya Soulja Boy na Chris brown kudondoshwa Dubai

  Share this

  Kwa taarifa hii inaonekana rasmi kwamba Soulja Boy na Chris brown pambano lao la ngumi kati yao bado lipo na limepangwa kupigwa pande za Dubai.

  Kupitia ripoti ambazo zimetolewa na mtandao wa Tmz zinasema kwamba Brown na Soulja Boy ni watu ambao wote hutoleana mapovu na wameamua kuliweka bifu lao kwenye pambano la ngumi, ila ishu kubwa ambayo wanaiitaji wawili hao kwenye pambano lao ni kuingiza mkwanja mrefu, Sasa Bad Newz pambano hilo halitofanyika USA ila Good Newz litadondoka Dubai.

  Wawili hao wameamua kulipeleka pambano hilo Dubai kutokana na vikwazo ambavyo wamekutana navyo hapo Las Vegas itakuwa mbinde kwao kuzichapa na ishu kubwa ikitajwa kuwa ni yale matumizi yao ya madawa kwamba hayatowawezesha kuruka vikwazo hivyo.

   

  Dondosha comments


  Share this