Rapper Jay-Z ameamsha mizimu ya wakongwe wa HipHop, hiki ndicho tunachosubiri

  Share this

  Baada ya Jay Z kuliamsha na Album yake mpya ya 4:44, Good Newz nyingine imedondoka kwa Dr Dre na Eminem kwamba mzigo wao mpya wa Album upo jikoni.

  Dr. Dre Reportedly Working On Eminem's New Album

  Director Allen Hughes aliumwaga mchele kupitia mahojiano yake na Uproxx kwa kusema kwamba mkongwe wa midundo mikali Dr Dre yupo mzigoni kuandaa project mpya ya rapper Eminem baada ya kutamba na Album yake ya  The Marshall Mathers LP 2.

  Katika maongezi yake, Hughes alisema “Dre bado anarekodi, watu hawafahamu hili ila Dre kila siku anarekodi, kwa kweli kila siku anarekodi nyimbo mpya, yaani unaweza mwita Picasso kwa hii staili, kila siku lazima achore, yaani muda huu anaproduce, ndani ya masaa 11 kuna ngoma ya Eminem anaitengeneza katika Album yake, kwahiyo Dre bado yupo active katika music” Alifunguka Hughes.

  Licha ya Aftermath/Interscope Records kutoongelea lolote kuhusu ujio mpya wa Album ya Eminem, bado tunaimani kwamba Director Hughes ni moja ya watu wa karibu wa Dre kutokana na kukaa muda mrefu kuandaa pamoja filamu ya The Defiant Ones.

   

   

  Dondosha comments


  Share this