RAPPER MEEKMILL MATATANI KUINGIA JELA MIAKA MIWILI

  Share this

  Rapper na mtaalamu wa kuchezea pikipiki kutoka marekani Meekmill yupo matatani kufungwa jela kwa miaka miwili mara baada ya kukutwa na mashtaka mawili mazito. Moja ikiwa ni kukamatwa mapema mwaka huu mwezi March akipigana katika uwanja wa ndege wa St. Louis, na shtaka la pili kukamatwa akiendesha chombo cha moto kwa kasi.

  Meekmill anaweza kufungwa jela kwa mashtaka hayo mawili ambapo kama atakutwa na hatia na makosa hayo Jumatatu hii ambapo kesi yake itasikilizwa. Kama imekuwa kawaida sana kwa Meekmill kukutwa na mashtaka mara kwa mara.

  Mkali huyo ambae ameshawahi kutoka kimapenzi na mwanadada Nicki Minaj huenda akawa anakutwa na mashtaka mengi ya kuendesha pikipiki kwa kasi kutokana na uzoefu wake mwingi wa kutumia vyombo hivyo yeye na kundi lake.

  Dondosha comments


  Share this