RAPPER T.I AIBUKA NA ISHU YA NELLY

  Share this

  Baada ya Akon kumtetea Msanii mwenzake Nelly kwa kusema kwamba Kwa jinsi anavyomfahamu Nelly, anaamini Nelly hawezi fanya jambo hilo.

  Sasa Mzee Mzima T.I naye ameamua kuongelea ishu hiyo kwa ujumla kwa kudai kwamba Wanawake huko nchini Marekani imekuwa kawaida kusingizia matukio kama hayo.

  Kupitia kurasa yake ya Instagram, T.I aliposti video akiwa ananyoa nywele zake, alifunguka kwa kuyataja majina ya wasanii kibao ambao walishawahi kushitakiwa na ishu kama hiyo ya Ubakaji ambayo mwisho inakuja kuonekana hao wanawake wanakuwa ni waongo.

  T.I alimtaja Mike Tyson, Tupac na watu wengine ambao wameshakumbwa na matukio kama hayo kusema kwamba ni ujinga, kutokana na wanawake wanaitaji kujipatia kitu kupitia majina ya watu hao mashuhuri, T.I anasema ameshachoshwa na matukio kama hayo ya kina dada kufanya mambo hayo.

  Dondosha comments


  Share this