Safisha macho kidogo kwa hii zawadi kutoka kwa Jay Z

  Share this

  Sio tu ngoma peke yake ndizo zinazofanya vizuri, ukidondoka upande wa video pia unakutana na vitu vilivyoshiba, Jay z kupitia Tidal wameachia kipande cha video ya ngoma ya “Kill Jay Z”.

  Baada ya Album yake mpya ya 4:44 kufanya vizuri na kushika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard 200 na kuifanya Album yake hii kuwa ya 14 kufika hapo, ukurasa wa Tidal wa Instagram umeamua kuwapa vionjo mashabiki wake kwa kushare kipande cha wimbo wa “Kill Jay Z” ambao unatarajiwa kutoka Julai 21 exclusive katika mtandao wa Tidal.

  #JAYZ's "Kill Jay Z" x 7/21 TIDAL TIDAL.com

  A post shared by TIDAL (@tidal) on

  Kama Wewe sio memba wa mtandao huo wa Tidal basi cha kufanya ni kutulia tu na kungojea pale itakapoachiwa katika mtandao wa Youtube.

   

  Dondosha comments


  Share this