Shetta ajipanga kusaidia Watoto Yatima msimu huu wa Ramadhan

  Share this

  Zimebaki wiki chache tu kabla ya kuingia katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, mwezi ambao wenye imani ya dini ya Kiislam na hata wasio waislam hujikita kwenye kufanya mema na kujiepusha na mabaya.

  Mkali wa Bongo fleva Shetta ametusanua kuwa msimu huu amejiandaa kutoa misaada kwa vituo vyote vya watoto yatima katika mikoa yote nchi nzima.

  Kupitia ukurasa wake wa instagram, Shetta ameandika kuwa Msimu wa Ramadhan unakaribia Mimi kama Shetta na menejimenti Yangu nzima napenda kukufahamisha kuwa kwa kidogo nilichonacho natarajia kuanza kusaidia na kutoa misaada kwa vituo vya watoto yatima na wenye uhitaji mkubwa mikoa yote ya Tanzania ambayo Ntaweza kuifikia,Naamini Vipo vituo vingi vyenye uhitaji mkubwa sana wa mahitaji ya kila siku.Hivyo basi popote ulipo kama unajua au unahusika na kituo chochote usisite kuwasiliana nasi kupitia;
  Social media( Instagram, Tiwtter, FaceBook; @OfficialShetta or @MxCarter )
  Email; shettamusic@gmail.com or MxCarter@slidevisuals.com
  Simu; +255 22 278 0288 / 0655653030
  Ili tuweze kukufikia kwa Urahisi Kabisa. #ShettaGivesBackToCommunity #RamadhanKareem #MunguWaKwetuSote?

  Kila la kheri katika mipango hiyo ya Shetta, Mungu amtie nguvu katika maadhimio yake hayo ya kusaidia watoto yatima.


   

  Dondosha comments


  Share this